MAPOKEZI YA MH. LOWASSA MKOANI KILIMANJARO
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za wanachama 33,780 wa
CCM Mkoa wa Kilimanjaro, waliomdhani ili aweze kupata ridhaa ya Chama
chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25, 2015. AAnaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM
Wilaya ya Moshi Mjini, Loth Ole Nesele.


Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja
na Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Juni 18, 2015, wakati shukrani
kwa udhamini wa kishindo alioupata kutoka wa WanaCCM hao, ili aweze
kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa
amepata udhamini wa wanaCCM 33,780.

Umati
wa wanaCCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, ukimshangilia kwa furaha, Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipopanda
jukwaani kuwashukuru wa kumdhamini kwa kishindo. Mh. Lowassa amepata
udhamini wa wanaCCM 33,780.

Sehemu
ya WanaCCM na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wamefurika katika
eneo la uwanja wa Ofisi ya CCM Mkoa huo wakifatilia kwa majini maelezo
ya Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa shukrani
kwa udhamini wa kishindo alioupata leo Juni 18, 2015.
Mh. Lowassa akisomewa Dua na Sheikh wa mji wa Moshi mara baada ya kupewa udhamini wa Kishindo katika Safari yake ya Matumaini.

Mchungaji akitoa maombi.
Wadau wakipata taswira ya Mh. Lowassa wakati akiondoka kwenye Uwanja wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro.
Vijana wa CCM wa Mji wa Muheza wakiuongoza Msafara wa Mh. Lowassa kwenye eneo hilo la Muheza kwa lengo la kuzumza nao.
Vijana
wa CCM Mji wa Muheza wakimshangilia Mh. Lowassa wakati walipomzimamisha
ili aongee nao, alipokuwa safarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro.
Ujumbe wa Vijana wa Muheza.
Ni furaha tupu.

























