SURA YA MKE YAMTISHA BWANAHARUSI
Duniani
kuna mambo, kuna vibweka na vibwakuro pia , twende sawa,Kang
Hu, mwenye umri wa miaka 33,aliwashtua wageni waalikwa siku ya
harusi yake, pale alipoamua kuwaomba radhi wakiwemo familia
yake na bi harusi Na Sung,mwenye umri wa miaka 30,kwa kumwambia
dhahiri shahiri kuwa ana sura mbaya na hafai kuolewa.
Bwana
harusi harusi huyo alikanganyikiwa mara baada tu ya kumwona bi
harusi wake kwa mara ya kwanza na kujaribu kujitosa majini.
Mara
akaamua kutoka eneo la tukio, kwenye ukumbi wa sherehe katika
mji wa Shiyan mji ulioko nchini China jimbo la Hubei na baadaye
alioneka akitembea kando ya mto akiwa na mawazo meeengi,mto
ambao alijirusha ndaniye mara moja.
Pal
Chan Wang alisema kwamba : familia ya bi harusi
ilivurugikiwa,familia ikashikwa na ghadhabu,na familia ya
mwanaume yao ikafura na marafiki zake walifadhaika mnoo kwa
matamshi yake .
Kang
alikuwa na uchaguzi wa bi harusi amtakaye na alikuwa
akilazimishwa kumuoa bi harusi huyo, ndo alipoamua kumfanyia
kituko hicho.
Wapiti njia ndio waliomgundua Kang mtoni ndipo walipowaita polisi na kuharakisha kushuka mtoni kumuopoa.
Qan
Tsui, mwenye umri wa miaka25, yeye ndiye aliyepiga picha hizi
anaeleza kwamba bwana harusi huyo alipojitosa mtoni alikuwa na
nguo zake zote na alikuwa akielea uso ukiwa unaelekea chini
kwenye maji,akiwa hajiwezi na mara nikasema anaweza kufa
asipopata msaada wa haraka.
polisi
walipowasili eneo la tukio,mmoja wao alijitosa mtoni na
kumdaka mara moja,na mwingine aliwarushia Kamba ili wamvutie
nje ya maji ya mto huo baadaye wamtoe maji yaliyoko kifuani.