Simba yapanga kumpa gari mchezaji bora wa timu hiyo
Uongozi
wa Klabu ya Simba umepanga kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo
katika sherehe za Simba maarufu 'Simba Day' inayofanyika kila mwaka
Agosti 8.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam, Rais wa Simba Evans Aveva alisema kuwa chini
ya uongozi wake wameanzisha tuzo hizo kwa wachezaji wa Simba ili kuibua
morali ya wachezaji na kuthamini mchango wao na hiyo imekuja baada ya
klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi kuingia mkataba wa miaka mitano na
Kampuni ya EAG ambao watakuwa na jukumu la kuiwezesha Simba kupata
mapato kwa njia mbali mbali ikiwemo udhamini kutoka makampuni mbali
mbali.
Aveva
alisema pia mbali na kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo pia
kutakuwa na tuzo ya mchezaji bora anayechipukia, kiungo, mshambuliaji
bora na mchezaji mwenye nidhamu.
"Mchezaji bora atapata gari, mchezaji bora chipukizi atapata Sh5 milioni waliosali watapata Sh2 milioni ikiwemo mwenye nidhamu.
Aveva
alisema pia mbali na tuzo hizo pia watatoa tuzo ya mchezaji aliyetukuka
'All Fame' ambaye nae atapata kiasi hicho cha fedha na pia mbali na
zawadi hizo wachezaji hao watapewa simu aina ya Huawei.
Mbali
na tuzo hizo Aveva alisema pia Kampuni hiyo ya EAG itakuwa pia na
jukumu la kuhakikisha Simba inafanikiwa mikakati yake ya kuongeza
mapato, kukuza namba ya wanachama, kuongeza na kuwapa faida wanachama wa
Simba kupitia huduma za Bima, kuongeza ari ya wachezaji Simba, kuwaenzi
na kukumbuka wachezaji wa zamani.
"Lengo
la utekelezaji wa mikakati hii ni kukuza ajira kutokana na biashara
zitakazoanzishwa, tunaamini tukitumia bidhaa za Simba ambazo tunalenga
kuzifikisha kila sehemu Tanzania na kutengeneza mfomo wenye lengo la
kuuipatia mapato stahiki tofauti na sasa.
"Kupitia
mkakati huu Simba itakuwa na uwezo wa kujenga uwanja wake na kuwa na
vyanzo endelevu vya mapato vitakavyoiwezesha kuboresha kiwango cha timu
na kuifanya iwe bora si Tanzania pekee bali Afrika nzima....: "Kwa timu
yenye mamilioni ya washabiki hili si jambo lisilowezekana bali
linalowezekana, ni jambo la kufurahisha na kuona uongozi wa Simba
umetambua hili."alisema Aveva.
Naye
mkurugenzi wa EAG Group Iman Kajura akizungumzia suala hilo alisema
"Kupitia mkataba huu nataka kuona Simba inapata mabadiliko makubwa ya
kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato, ili iache kutegemea
mapato ya mlangoni na ada za wanachama pekee."
Kajura
alisema mipango yote ya kuendesha zoezi hilo anaipata kutoka klabu ya
Arsenal ya England ambayo anafanya nayo kazi katika kukuza na kuingiza
wabia wa biashara.