Jimbo la California kukabiliana na ukame
Serikali
ya jimbo la California nchini Marekani limetoa amri ya kudhibiti
matumizi ya maji katika jimbo hilo kwa mara ya kwanza katika historia
yake ya kupambana na ukame.
Gavana wa jimbo la California, Jerry Brown analenga kupunguza matumizi ya maji kwa asilimia ishirini na tano.
Mamilioni
ya mita za mraba za viwanja vya nyasi zinazotunzwa vizuri katika ardhi
inayomilikiwa na serikali zitabadilishwa na kuwekewa majani yanayohimili
ukame.
Gavana
Brown ameyasema hayo katika mkutano wa waandishi wa habari katika milima
ya Sierra Nevada ambayo haina nyasi ambayo kwa kawaida wakati huu wa
mwaka ingekuwa imefunikwa kwa theluji yenye kuzidi mita moja kwenda juu