Bawacha Arusha wameitaka tume ya uchaguzi kuwa makini
Baraza
la wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema (Bawacha) mkoa
wa Arusha wameitaka tume ya uchaguzi na viongozi wake kuwa makini
katika uchaguzi mkuu ujao na kujifunza mfano wa demokrasia ya kweli kwa
tume ya uchaguzi ya Nigeria kwa kutangaza matokea halisi ya
uchaguzi bila kupendelea chama tawala ili kuepusha migogoro ya kisiasa kama inayo endelea kushamili katika baadhi ya nchi za Afrika. Mwenyekiti wa Bawacha Arumeru mashariki na mbunge wa viti maalum Rebeca Mgodo ametoa kauli katika mkutano wa vionozi wa bazara la wanawake wa Chadema Arumeru mashariki ambaye amesema umefika wakati wa tume ya uchaguzi ya Tanzania kuiga mfano wa tume za nchi ambazo demokrasia yake imekuwa kama Nigeria tofauti na tume ya uchaguzi ya Tanzania ambayo inafanyakazi kwa kuibeba serikali na chama tawala na kukandamiza wapinzani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Arusha Sesy Ndosi amesema wakati umefika wa wanawake kuongoza mabadiliko katika taifa kwa kuingia katika uonogozi huku akiwataka waache kutegemea nafasi za upendeleo na badala yake wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi mkuu ujao kugombea ili kuondoa viongozi visiki wasiyo jali mali za umma huku wajumbe wengine wakieleza umuhimu wa wanawakekatika uongozi.(KILONGE)