Al Shaabab na chimbuko la ugaidi ( Uchambuzi)

1_b40ad.jpg

TUMESHAJADILI maana ya ugaidi na aina za ugaidi kwa kuzitolea mifano. Hapa tutajadili juu ya chimbuko la ugaidi na kwa kutoa mifano.

Wa- Salote
Kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita kikundi cha Wayahudi kilipambana vikali
dhidi ya himaya ya Waroma katika iliyokuwa Palestina ya zamani. Kikundi
hiki kiliitwa Salote. Ni wenye hasira kali ikiwa na maana pia kuwa kilikuwa ni
kikundi cha kisiasa na kidini chenye imani kali. Kikundi hiki kilitaka
Wayahudi wote wazingatie yote kulingana na maagizo ya dini yao.
Wasalote walipambana kisiasa dhidi ya dola ya wavamizi ya Waroma.
Wasalote waliongozwa na Myahudi Galileo, ambaye amri yake ya kuwataka
wafuasi wake kugoma kulipa kodi ndio ilikuwa chachu ya kuanzisha mapambano
ya kigaidi dhidi ya wavamizi wa Kiroma. Jambo hili linashuhudiwa pia katika
maandiko matakatifu ya Biblia juu ya kodi katika Agano Jipya.
Hatma ya Wayahudi haikujulikana , lakini, kiongozi mpya alijitokeza
na kuwaahidi Wayahudi ukombozi kutoka kwenye mikono ya wavamizi. Hatimaye,
baada ya machafuko yaliyodumu kwa miaka sabini, Wasolote waliangamizwa
baada ya Jerusalem kutekwa na hekalu kuangamizwa. Wasalote walirudi nyuma
hadi kwenye vilima vya Masada.
Baada ya kushindwa huko kwa Wasalote, Wasalote wapatao elfu moja
walijiua kwa pamoja. Wasalote waliwaua kwanza wanawake , watoto na wazee,
baadae wanaume nao walijiua kabla ya Waroma hawajavitwaa vilima hivyo.
Inasadikiwa tukio hili lilitokea mwaka 73 baada ya Yesu Kristo.
Wa-Assassine
Miaka elfu moja baadae lilijitokeza kundi jingine la kigaidi, hawa waliitwa
Assassine. Hawa walikuwa wafuasi wa dhehebu la dini ya Kiisamu lililokuwa
na makao yake makuu katika Iran ya leo. Kutoka huko Iran walimtuma kiongozi
wao aliyeitwa Hassan Ibn Sabah, aende katika Mashariki ya Kati yote. Huko
akafanye mauaji ya kulipwa.
Wafuasi wa dhehebu hili walifahamika pia kwa kuvuta bangi kabla
hawajafanya tendo la kigaidi kwa jina la Mungu. Hapa tunaona neno
"Assassin" kwa Kiingereza na hata kwa Kifaransa, lina maana ya "kuua."
"Assasination" kwa Kiingereza, na kwa lugha ya kiarabu linamaanisha "
Mla-bangi". Wa-assassin walikuwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia. Vitendo
vyao vya kigaidi viliwalenga zaidi Wasuni waliochukua sehemu kubwa ya
Persia.
Kunako mwaka 1200 vitendo vya kigaidi vya Wa-assasasine vilikoma
baada ya mjuukuu wa Djingis Khan kuangamiza ngome na makao makuu ya
Wa-assassine. Huu ni uchambuzi endelevu...
Maggid,
Iringa.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.