AKON KUMTANGAZA RASMI MSHINDI WA SHINDANO LA AIRTEL TRACE STARS AFRICA APRIL 18, 2015
Dar
es Salaam, 13 April 2015 Finali ya shindano la Airtel Trace Music Stars
Afrika lililoshirikisha washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika chini ya
majaji mahiri akiwemo Akon, Devyne Stephens na Lynnsha mwisho mwa wiki
hii watashirikiana kumtanga rasmi mshindi wa Airtel Trace Afrika.
Airtel
kupitia taarifa yake iliyotumwa na ofisa uhusiano wake Jane Matinde
imesema “Shughuli nzima ya kumtangaza mshindi itaonyeshwa kupitia chanel
ya Trace inayopatikana katika kituo cha DSTV #325 siku ya jumamosi
tarehe 18 April 2015
Shindano
hilo kabambe la Airtel Trace music star lilihusisha washiriki wengi
walioshiriki kupitia kupiga simu na kurekodi mojakwa moja ambapo jumla
ya simu zaidi ya milioni mbili na laki tatu za washiriki wote zilipigwa
na kufanya namba ya washiriki wa shindano hili kubwa Afrika kuweza
kuzidi mashindano ya Ulaya na marekani kama vile ya voice na idols.
Washiriki
13 kutoka nchi za Afrika waliingia katika kinyanganyiro cha kutafuta
mshindi tarehe 28 machi 2015. Usikose kushuhudia shindano hilo la
kusisimua lenye vionjo vya kila aina, mbwembwe na bashasha tele.
Finali
hizi za Airtel Trace Stars zitaonyeshwa siku ya Jumamosi ambapo
watazamaji na majaji watachagua na kutangaza mshindi ambaye atapata dili
la kurekodi , kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa mwanamuziki nguli wa
nchini Marekani lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500,000/=
Progam
hii ya finali itarushwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18 April kuanzia saa
tatu Usiku na kurudia siku ya Jumapili tarehe 19 Aprili kuanzia saa
kumi jioni katika chaneli ya Trace urban. Kipindi kitadumu kwa muda wa
dakika tisini.
