YANGA YAFUNJA MWIKO MKWAKWANI WAICHAPA MGAMBO SHOOTING GOLI 2-0

Katika
mchezo huo yanga iliwabidi wangoje mpaka dakika ya 76 kuandika goli la
kuongoza lililotiwa kimiani na Saimon Msuva baada ya kutokea piga ni
kupige golini mwa Mgambo Shooting.
Goli la pili lilipatikana katika dakika ya 83 kupitia kwa Amisi Tambwe aliyeunga kwa kichwa krosi ya Saimon Msuva na kupelkea yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-0 ikiwa ni sawa na magoli aliyofungwa Simba SC katika uwanja huo na Mgambo shootingi siku ya jumatano.
Kama ilivyoada kwa michezo inayochezwa katika uwanja huo kutawaliwa na mipira ya juu, na kukiwa na ufundi mdogo kwa timu zote mbili katika mchezo wa leo, huku kukiwa hakuna timu iliyolemewa katika mchezo huo.
Kilicho wagharimu Mgambo shooting ni kitendo cha kuamua kuzuia zaidi katika kipindi cha pili kulinganisha na kipindi cha kwanza ambapo walipandisha mashambulizi ya kutosha lakini hawakuweza kupata goli lolote lile.
Kwa matokeo hayo yanga wamefikisha point 37 wakikwa katika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 18, wakati Azam FC wakiwa katika nafasi ya 3 wakiwa wamecheza michezo 17 na pointi 33.