POLISI WAMUOKOA MSUVA TAIFA
Simon Msuva akisindikizwa na
askari kupanda usafiri wa kumuondoa eneo la uwanja wa Taifa jana baada
ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba,
uliomalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0, na kufanya mashabiki kumzingira
wakitaka kumpiga wakimtuhumu kuuza mechi hiyo na kucheza chini ya
kiwango.
*********************************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
MCHEZAJI
wa Yanga, Simon Msuva, amenusurika kupewa kichapo kutoka kwa mashabiki
wake na kuokolewa na Polisi, baada ya mchezo wa jana kumalizika.
Msuva,
aliyekuwa wa mwisho kutoka ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo, huku
wachezaji wenzake wote wakiwaa tayari wameshaingia ndani ya basi lao,
alizongwa na mashabiki huku wakimsemea maneno makali na kutishia
kumtwanga wakidai kuwa ameuza mechi.
Winga
huyo, aliokolewa na Polisi walioanza kuwatawanya mashabiki hao kwa
virungu, huku wengi wakimshika mkono Msuva na kumuweka kati ili
kumfikisha kwenye usafiri ili kuondoka eneo hilo.
Askari
hao pia walionekana kuchanganyikiwa huku wakimuongoza mchezaji huyo,
kuelekea pasipojulikana huku wakitafuta basi la timu wakati tayari
walishalipita na likiwa na ukubwa ambao kamwe huwezi litafuta kama gari
ndogo.
Vurugu
hizo ziliendelea huku mashabiki wakimfuata Msuva, wakimtukana huku pia
askari hao wakijitahidi kuwatawanya kwa virungu, wakiendelea kutafuta
basi la timu hadi alipofika Salum Telela na kumshika mkono kumuelekeza
basi lilipo na kuelekea katika basi akiwa chini ya ulinzi.
Baada
ya Msuva kupanda basi hilo lilianza kuondoka mahala hapo mashabiki
wakilifukuza huku wakiendelea kutukana matuzi na kumtuhumu Msuva kwa
maneno kuwa ‘eti’ ameuza mechi.
Chini ya ulinzi mkali.
Wakitafuta Basi la wachezaji
Mashabiki wakimzonga Msuva
Wakirejea kupanda basi la wachezaji baada ya Telela kumfuata na kumwonyesha basi lilipo.
Wakielekea kwenye basi hilo.
Wakimpandisha basi




