Matokeo ya uchaguzi Nigeria leo jioni
Matokeo ya uchaguzi Nigeria leo jioni
Mama akipiga kura nchini Nigeria
Wasimamizi wa uchaguzi wakiwahakikika wapiga kura kabla ya kupiga kura zao.
Mkuu wa
Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza
mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni.
Upigaji
kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea
hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi
ya wapiga kura.
Mama
akipiga kura nchini NigeriaKauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume
Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa
tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi
ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko
ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika
jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka
jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi."
Bwana
Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna
Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa.
Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa
kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa
bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana
tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine
wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana
na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.",
amesema Jega.
Wasimamizi
wa uchaguzi wakiwahakikika wapiga kura kabla ya kupiga kura
zao.Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha
kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa
Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa
Nigeria kukubali matokeo.
Uchaguzi
nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili
wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na
Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka
ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa
kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.CHANZO:BBC