MAAJABU HAYA>>>JIONEE SIMU ILIYOTENGENEZWA KWA MAJANI, VIDEO IKO HAPA ANGALIA
Teknolojia
inatufungulia mapya kila siku.. Nakumbuka simu za kwanza za mkononi
zilikuwa kubwa halafu nzito, baadae ikaja fashion ya simu
ndogo ndogo, zile kubwa watu wakawa wanaziita ‘mshindi’ ambalo ni jina
la sabuni… Sasa hivi tunaona fashion ya simu kubwa inarudi mdogomdogo.
Sean Miles anaingia
kwenye historia, anaingia kwenye headlines pia.. yeye kagundua hii
simu ambayo imetengenezwa kwa majani kabisa pamoja na mchanganyiko wa
vitu vingine vilivyochakaa ama vilivyoharibika.
Dili ambayo alipewa na Kampuni ya O2 ilikuwa Miles afanye
ubunifu njia ambayo wataweza kutumia mabaki ya vitu ambavyo vimechakaa
na havifai kwa matumizi, katoka na hii ambayo hata waliomuagiza hiyo
kazi imewashangaza yani.
Unaambiwa cover ya simu hii ukiiangalia ni kama majani kabisa.
Ubunifu huu umefungua ukurasa mpya kwenye Teknolojia, Kampuni ya O2
wanaangalia kama wataweza kuweka nguvu nyingi zaidi ili simu zenye
cover hizi zilizotengenezewa majani zitengenezwe nyingi na kuingia
kwenye soko la Dunia.
