LOWASSA AZIDI KUHAMASIKA JUU YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS, AWAHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWA WINGI DAFTARI LA WAPIGA KURA
Mbunge
wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia
ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda
boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani
kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa
taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea
nafasi ya Urais.
Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu.Aidha
na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao
vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari
la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki
katika uchaguzi kwa kupiga kura.
Wanafunzi
hao zaidi ya 300 walifika nyumbani kwake hapo majira ya saa sita
mchana na kuzungumza nae na kufikisha salamu zao ikiwa ni pamoja na
kumchangia fedha za kuchukulia fomu.

