KINANA-WANANCHI WA KARATU WANA HAKI YA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI ZA MAENDELEO KAMA WENGINE.
Hata
hivyo Kinana amesema wananchi wa Karatu ni Watanzania na wana haki ya
kupata huduma mbalimbali za maendeleo na serikali ya CCM haitawaacha
kama wanavyoachwa na viongozi wao wa CHADEMA waliowachagua wenyewe.
Kinana
akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako
kwenye ziara ya siku tisa ya kikazi mkoani Arusha wakihimiza na kukagua
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ikiwemo na kusikiliza matatizo
ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi,hata hivyo katika wilaya ya Karatu
imeonekana kukwamishwa na Mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Israel Natse
Chadema, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na madiwani kwa kuitenga
baadhi ya miradi ambayo ipo katika vijiji ambavyo madiwani na wenyeviti wa vijiji wanatoka Chama cha Mapinduzi CCM ambapo wananchi wa kijiji hicho wamemlalamikia Kinana.
Baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo uwanjani hapo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa Karatu
waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo wa hadhara
Baadhi
ya wananchi wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa na Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano huo wa hadhara.
Wananchi
wa kijiji cha Baray-Mbuga Nyekundu wakimshangilia Katibu wa NEC
Itikadi na uenezi,Nape Nnauye alipozungumza kabla ya Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana kushiriki ujenzi wa jengo la kituo cha upasuaji afya .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Baray.






