Kane kuanza mechi ya kirafiki
Mshambuliaji
wa Tottenham Harry Kane anatarajiwa kuanza katika mchezo wa kirafiki
utakaopigwa leo katika dimba la Juventus Stadium mnamo saa tano kasorobo
kwa saa za Afrika Mashariki huko nchini Italy.
Mchezaji
huyo kinda ambaye amekwisha tikisa nyavu mara 29 katika msimu huu akiwa
na klabu yake ya Spurs, alitumia sekunde 79 tu kufunga goli baada ya
kuingia akitokea benchi kuziba pengo la nahodha wake Wayne Rooney katika
mchezo wa kufuzu dhidi ya Luthuania siku ya Ijumaa ambapo England
ilishinda kwa jumla ya mabao 4-0. ''Harry anastahili kupata nafasi''
alisema kocha wa England Roy Hodgson. '' Hii ni nafasi kwa baadhi ya
wachezaji kuonesha kuwa wanaubora'' aliongeza kocha huyo.
Mpaka sasa mchezaji huyo amekwisha funga mabao 8 katika michezo 10 aliyoichezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21.
Wakati
hayo yakijiri Wayne Rooney amebakiza mabao mawili tu ili kufikia rekodi
ya mfungaji wa wakati wote wa timu ya taifa England Sir Bobby Charlton
ambaye aliweka kimiani mabao 49 katika kipindi chake cha uchezaji.CHANZO:BBC