Giroud aipaisha Arsenal EPL ugenini

MABAO
mawili ya Olivier Giroud, dakika ya 24′, 28′ yametosha kuipa Arsenal
ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Newcastle United kwenye mechi ya
ligi kuu England. Bao la Newcastle lilifungwa na Moussa Sissoko katika
dakika ya 49′. Ushindi huu kwa Arsenal unakuja baada ya kutolewa UEFA
jumanne ya wiki hii kwa wastani wa mabao 3-3 dhidi ya Monaco. Mechi ya
kwanza walifungwa 3-1 Emirates na mechi ya pili wakashinda 2-0 nchini
Ufaransa na Monaco wakasonga kwa faida ya goli la ugenini.
MATOKEO YA MECHI ZILIZOMALIZIKA England – Premier League March 21(P.T)
FT Manchester City 3 – 0 West Bromwich Albion
FT Aston Villa 0 – 1 Swansea City
FT Newcastle United 1 – 2 Arsenal
FT Southampton 2 – 0 Burnley
FT Stoke City 1 – 2 Crystal Palace
FT Tottenham Hotspur 4 – 3 Leicester City
FT West Ham United 1 - 0 Sunderland