BONDIA MOHAMED MATUMLA AMTANDIKA KWA POINT BONDIA WANG XIN HUA KUTOKA CHINA
Mwamuzi
wa Mpambano wa Masumbwi uliowakutanisha mabondia Mohamed Matumla
(Tanzania) na Wang Xin Hua (China) katika Ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es salaam usiku huu,akiwa amemnyanyua mkono Bondia Mohamed
Matumla baada ya kumchapa kwa Point bondia mwenzake kutoka nchini China
katika mpambano wa raundi 10 wa kuwania nafasi ya kucheza katika pambano
la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi
wengi wa masumbwi Duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na
Manny Pacquiao unakaochezwa mapeka mwezi Mei mwaka huu, huko nchini
Marekani.
Wanahabari wakichukua taswira mbali mbali za mpambano huo.
Bondia
Mohamed Matumla akiangalia namna ya kumrushia konde mpinzani wake Wang
Xin Hua (China) wakati wa mpambano wao wa raundi 10 wa kuwania nafasi ya
kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na
unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi Duniani kati ya
mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapeka
mwezi Mei mwaka huu, huko nchini Marekani.Katika Mpambano huu, Bondia
Mohamed Matumla alishinda kwa point.
Matumla akimchezesha Wang Xin Hua.
Wang Xin Hua akirusha konde kwa Mohamed Matumla ambaye leo alikuwa makini sana kuhakikisha hampi point hata moja mpinzani wake.
Matumla anatakata hapa,anampa ambakati moja maridadi kabisa.





