MWANAMKE FAHAMU NJIA KUUKUMI (10) ZA KUMFANYAMWANAUME AONGEZE MAPENZI NAKUKUHESHIMU
.
1. Vaa vizuri (look sexy) pindi unapokuwa nae hii itamfanya aendelee kukuona mpya kila siku.
2.
Jiheshimu, mwanamke unapokuwa unajiheshimu hata mwanaume pia
hukuheshimu na haitakiwi ujirahisishe pindi unapokuwa nae jua thamani
yako kama mwanamke.
3.
Tumia muda wako na marafiki zako au kukamilisha malengo yako binafsi.
Hii itafanya mwanaume akukumbuke sana pindi unapokuwa haupo na kukupigia
simu mara kwa mara.
4.
Kuwa na maisha yako usimtegemee mwanaume kwa asilimia 100, hii
itamfanya asikukandamize kwa kujua bila yeye wewe huwezi kusimama,
mtegemee
pale tu unapozidiwa.
5.
Uwe mbunifu kitandani, hii itamfanya mwanaume akukumbuke kwa utashi
wako na kumfanya asijisikie kutoka nje ya mahusiano, usiwe gogo utaboa.
6.
Kuwa mwanamke makini hasa kwa kujihusisha na vitu mbalimbali vya
kijamii na taharifa mbalimbali zinazoihusu jamii visikupite ili kuendana
na dunia ya sasa.
7.
Jitume sana katika kazi hasa wakati anapokuchukulia poa. Kamwe usimpe
nafasi mwanaume wako akuone kama wewe wa ziada kwake jitume kiasi kwamba
awe anakuogopa.
8. Jenga mazingira ya kuonyesha kwamba unamkubali mbele ya kadamnasi hii itamfanya ajione mwenye bahati kuwa na wewe.
9. Muepuke pindi anapokukosea heshima usijibizane nae na pia usijibu “message” wala kupokea simu
kama adhabu na pia kupunguza hasira, hii itasaidia kwa yeye kujirekebisha.
10. Fata ndoto zako mwenyewe, kuwa mvumilivu kuhusu maisha na malengo yako. Ukiwa ni mtu wa
kubadilika badilika, hueleweki na wala hujui usimame upande gani mwanaume atashindwa kukuheshimu.
