Kumbe Ngasa hapati chochote yanga alia njaa tu mtaaani
10th February 2015
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Sudan na Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati walimuhitaji Ngasa kwa dau la Dola za Marekani 150,000 (Sh.
milioni 269), lakini Ngasa chini ya ushawishi wa viongozi wa Yanga
alikataa ofa hiyo na kurejea Jangwani baada ya mkataba wake wa mkopo wa
kuichezea Simba kumalizika.
Ngasa ametoa kauli hiyo kufuatia kukatwa "fedha zote za mshahara"
kwa ajili ya kulipia deni la Sh. milioni 45 ambazo alikopa benki mwaka
jana.
Akizungumza jana na gazeti hili, Ngasa, alisema kuwa kwa sasa makato hayo yanamuumiza lakini hana la kufanya.
Alisema katika maafikiano, Yanga walimwambia watamkata Sh.500,000
kwa mwezi lakini ghafla walikiuka makubaliano na kuanza kumkata Sh.
milioni moja kabla ya miezi miwili iliyopita kumkata pesa zake zote.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar ya mkoani Kagera na
Azam ya jijini Dar es Salaam alisema kuwa anavumilia 'maumivu' hayo
lakini bado anaamini milango ya yeye kwenda kucheza soka la kulipwa nje
ya nchi bado haijafungwa kwa vile mkataba wake unaelekea kumalizika
Yanga.
"Najuta kwa kukataa kwenda El Merreikh. Simba na Azam wanisamehe,
walitaka kunipeleka huko lakini nilikataa na kwa mapenzi yangu nikaamua
kurejea Yanga, sasa naumia, ila naamini kila jambo lina mwisho, deni
nitamaliza kulilipa. Nilikopa mwenyewe na Inshallah nitamaliza
kulilipa," alisema Ngasa.
Mshambuliaji huyo ambaye pia yuko katika kikosi cha timu ya soka ya
taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na ambaye aliwahi kufanya majaribio ya
kucheza soka la kulipwa katika klabu ya West Ham United ya Uingereza na
Vancouver Whitecaps ya Ligi Kuu ya Marekani akiitumikia klabu hiyo ya
MLS katika mechi ya kirafiki dhidi ya Manchester United, alisema
anaamini bado ana kiwango cha kucheza soka la kimataifa.
Aliongeza kwamba juhudi zake binafsi ndiyo zinamsaidia kuonekana mchezaji mzuri na ataendelea kujituma ili kutimiza ndoto zake.
Magoli hayo ya Ngasa yaliisaidia Yanga kulipa kisasi cha kufungwa
2-0 dhidi ya Mtibwa katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu
ya Bara na kupanda kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 25, tatu juu ya
Azam walio na mechi mmoja mkononi.
Kikosi cha Yanga sasa kiko kambini kwa ajili ya kujianda na mechi
yake ya hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF IX kutoka
Botswana itakayofanyika Jumamosi Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa.
CHANZO:
NIPASHE
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI