KAULI YA OBAMA KUHUSU UKRISTO YAZUA KIZAAZAA
Kauli
ya Rais Barack Obama ya kuwataka Wakristo kujua kuwa Uislamu si dini
pekee inayohusishwa na vurugu na mauaji, imezua kizaazaa duniani na
baadhi wameanza kuhoji kama kiongozi huyo wa kwanza mweusi wa Marekani
ni Mkristo.
Obama
alitoa kauli hiyo Jumatano wakati wa Siku ya Taifa ya Maombi (National
Breakfast Prayer) alipofananisha Vita vya Msalaba na vitendo vya ugaidi
vinavyofanywa na vikundi vya Kiislamu vyenye imani kali.
"Hadi
tutakapokuwa juu ya farasi na kufikiri kuwa jambo hili ni la pekee kwa
baadhi ya sehemu, kumbuka kwamba wakati wa Vita Vitakatifu (crusades) na
Mahakama ya Kanisa Katoliki (Inquisition), watu walifanya vitendo vya
kutisha kwa Jina la Kristo," Obama alikaririwa na Shirika la Habari la
AFP akizungumza kwenye hafla hiyo Jumatano.
"Na katika nchi yetu, utumwa na sheria za kibaguzi (Jim Crow), zote pia zilihalalishwa kwa jina la Kristo."
Obama
alikuwa akitoa hotuba yake kuhusu dini kwenye hafla hiyo iliyofanyika
Washington, D.C. Akitumia maandiko ya dini za Kiislamu, Kiyahudi na
kikristo, Obama alisifu imani yake.
"Utamaduni
wa maombi umetuweka pamoja, ukitupa nafasi ya kukusanyika kwa
unyeyekevu mbele ya Mungu na kutukumbusha nini kinatakiwa kushirikiana
kama watoto wa Mungu," alisema.
Obama
pia aliwageukia magaidi wa kijihadi aliosema "wanaasi Uislamu".
Alilinyooshea kidole kundi la Islamic State ambalo alisema "limefanya
vitendo visivyoweza kutamkwa vya ukatili " Mashariki ya Kati pamoja na
wanamgambo ambao hivi karibuni waliua watu kadhaa kwenye ofisi za gazeti
la vibonzo la Charlie Hebdo nchini Ufaransa.
Lakini kauli yake imekosolewa sehemu mbalimbali.
Katibu
wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Padri Saba
Raymond alisema alichozungumzia Obama ni historian a hivyo dunia
inatakiwa ijifunze.
"Kama
kimetokea, kimetokea. Tunatakiwa kujifunza kutokana na kilichotokea.
Katika ulimwengu wa sasa ni fursa ya kujifunza yale yaliyotokea na
hayafai na wakati huu yasitokee tena... wale wanaoyataka, washindwe,"
alisema Padri Raymond
Padri
Raymond aliongeza kusema: "Utumwa ulikuwa haufai na Marekani
walijihusisha kwa hili (kuuondoa) na hii ni historia ambayo wanapaswa
kuiacha."
Profesa
wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho alisema:" Ni kauli ya
kujihami na anaogopa kuwanyooshea kidole moja kwa moja... Wamarekani
wasingependa yatokee kama yaliyowahi kutokea huko nyuma.