JERISLAA AMKANA MWALIMU NYERERE NA SERA ZAKE
Sio kila alichokichukia Mwl. Nyerere lazma ukichukie...... Kila mara
huwa napenda kumtembelea Baba yangu na kuzungumza nae mambo mbalimbali.
Lakini huwa hatuna msimamo wa pamoja wa jambo lolote lile, zamani
tulikuwa tunabishana sana. Sikuhizi namsikiliza zaidi na kujengea hoja
yake ninayoamini. Mara zote tunakubaliana kutokukubaliana. Mwl.Nyerere
alikuwa na fikra zake alipoiongoza Tanzania, kwa wakati wake yalikuwa
ndio maamuzi yake. Nationalization na free social service. Serikali
ilifanya biashara. Mzee Mwinyi alikuwa na fikra zake, biashara ikapanuka
na wananchi wakaanza kupata bidhaa zilizokuwa adimu. Mzee Mkapa
amefanya yake, Privatization na tukaona sekta binafsi ikikuwa,kutoa
ajira na KULIPA KODI. Dr.Kikwete ameendelea kuboresha miundombinu, umeme
vijijini(ambao ni mpango wake na Waziri yeyote akija utaendelea) na
serikali yake imeongeza sekondari kwa 500% ambazo sasa tunazijengea
maabara. Viongozi wote hawa waliongoza kwa muda wao na kufanya maamuzi
kwa kipindi kile. Naamini kila mmoja ana fursa ya ku-challenge hasa
ukizingatia mtazamaji mpira anaona zaidi ya mchezaji ("angepiga vile au
hivi"). Sikuwahi kumwona Babu yake Baba na wala sijui habari zake, babu
yangu yupo zaidi ya story sijajifunza mengi. Baba yangu yupo na
tunaelewana sana ila mitazamo yetu mingi ni tofauti. Binafsi
sifurahishwi sana na kauli "Kama Mwalimu angekuwepo" au "Kama Mwalimu
angefufuka" naamini viongozi walioko wana cha kujifunza kwenye historia
na yao ya kuamua kwa nyakati zao. Wanafunzi wa Sheria tunasoma majaji
wakitofautiana mtazamo kwenye kesi moja yenye facts sawasawa. Sio kila
aliyemchukia Mwalimu,lazma nawe umchukie kwa sababu zilezile........
