Hizi Ni Sababu Kuu Tano Kwanini Lowassa Anafaa Kuwa Rais 2015.....soma zaidi=====>>
Maisha
ya watanzania yamekua magumu mno,sasa sukari ipo juu ikiwa ardhi na
mabonde kama ruvu mtibwa na kageara tunayo, umeme usio wa uhakika wakati
gesi ya mtwara na RUBADA, madawa hakuna hospitalini, viongozi
wanatuziba masikio kwa vizungumkuti vya ESCROW huku madawati hakuna
shuleni, vitendo vya kihalifu vimejaa kila kona watu wakisaka ridhiki
kwa nguvu, tumaini la katiba mpya ni kizunguzungu kiasi kutuacha wakiwa
Zaidi sisi masikini wakitanzania, huku tukijengewa chuki na serikali na
watawala kwa upenyo wakushuka uzalendo na kiasi cha kusema watu
kuikimbia nchi kwa vijana ni kawaida kutafuta maisha ughaibuni na kusema
hii nchi sasa si ile ya NYERERE bali ni ya watawala makatili mno.
Lakini kwa muktadha ule ule wa kidemokrasia ambao hata rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania awamu ya tatu Mh. Benjamin Mkapa aliyasema pale
alipo chagiza kabla kuteuliwa Dk Jakaya Kikwete ndani ya CCM kuwa
achaguliwe mgombea ambaye vijana na wapiga kura wengi wanamtaka kitu
ambacho kilipelekea Dk. Kikwete kushinda kwa kishindo ndani ya chama na
hata katika uchaguzi mkuu 2005. Sasa zifuatazo ni sababu ambazo Lowassa
atapitishwa kugombea URAIS kwani wanachama na watanzania wanamuhitaji.
1.MRITHI SAHIHI WA MWL. NYERERE KATIKA VITA DHIDI YA UJINGA
Edward
Lowassa ni mwana siasa Pekee ambae ndani ya CCM,anaefaham Vission ya
Mwalimu Nyerere 1961 Mwalimu alitangaza maadui watatu (1)Ujinga
(2)Maradhi (3) Umasikini. Mwalimu katika miaka yake 24 alisimamia swala
moja Elimu ya Kujigetemea na baada ya kuondoka mfumo huu uliharibika,Ili
kupambana na Adui hao Mwalimu alianzisha Vijiji vya Ujamaa,msingi hapa
ili kuongea Uzalishaji,huduma ya afya na Shule, akajenga shule za msingi
katika kila kijiji. Mwaka 2005 Edward Lowassa aliamua kufufua upya
utekelezaji wa Dira ya Mwalimu nayo ni kuwekeza kwenye Elimu na
Kupambana na maadui 3.Alisimamia Ujenzi wa Miundo Mbinu ya Elimu kila
kata( sekondari),Kupanua elimu ya Chuo Kikuu, Kusukuma Ujenzi wa vyuo
vya kada ya kati (Veta) ili kujenga Kada la kati ya wataalam wa Ufundi
mbali mbali, Kupanua Vyuo vya Ualimu ili kuziba pengo la upungufu wa
waalim,mambo haya hayana tofauti mapambano alianzisha Mwl Nyerere baada
ya uhuru kupambana na maadui watatu. Elimu imekua Agenda kuu ya Edward
lowassa,Anaamini katika hilo Jambo kuwa msingi wa kupambana na
Umasikini,Elimu itasaidia Uzalishaji,Elimu Itapambana na Maradhi,Elimu
Itaondoa Ujinga miongoni mwa Jamii yetu, hii ni sababu pekee itakayo
ifanya CCM kumpitisha kurudisha taswira ya chama.
2. MAAMUZI MAGUMU NA MAKINI KATIKA UONGOZI
Kwa
kipindi kirefu sasa ndani ya nchi yetu tuna tatizo la maamuzi katika
utekelezaji wa sera za serikali, viongozi wamekuwa wazito mno kutekeleza
makubaliano ya vikao vyao wakiogopana au hata rushwa kutawala miongoni
mwao hivyo kushindwa kutekeleza maamuzi hayo. Edward Lowassa ni kiongozi
ambaye kwa kipindi chake alicho kuwa madarakani ameonyesha kuwa si
kigeugeu kwa maana ya kwamba mara zote ambazo baraza la mawaziri katika
vikao vyake vya ndani walipo fika makubaliano yeye alitekeleza,
Utekelezaji wa ujenzi wa chuo kikuu Dodoma. Taarifa za ndani za viongozi
zilionyesha ugumu mno wa utekelezaji wa sera hii ya chama, Lowassa
ilifikia hatua kuwaeleza viongozi mbalimbali waandamizi katika ngazi za
maamuzi na utekelezaji kama yeyote anaona ujenzi wa chuo kile
hauwezekani aandike barua ya kujiuzulu na akabidhi kwake ampatie Rais
Dk.Jakaya Kikwete, kitu ambacho kiliongeza ujasiri wa utekelezaji wa
sera na sasa tunaona watoto wa masikini wakipata elimu. Alivunja mkataba
wa city water, mkataba ambao ulifanya serikali kushtakiwa lakini na
hata kuleta nafuu katika upatikanaji wa majia ndani ya jiji la dar es
salaam pia bila kusahau alivunja mkataba wa kimataifa katika usambazaji
wa maji kanda ya ziwa kitu kilicho mfanya mpaka aogepeke na jumuia za
kimataifa akiwa anatetea haki ya Mtazania kwa hakika ni mzalendo na mtu
pekee ndani ya CCM hii ya DK. Jakaya na Kinana anaefaa kuipeleka dira ya
taifa mbele.
3. MPAMBANAJI ALIAZIMIA KUFUTA UMASIKINI
Lowassa
ni Mwana siasa Pekee ndani ya CCM ambae Anaamini UMASIKINI si sifaa
bora kwa Mtanzania kujisifia,Umasikini si Sifa ya Kiongozi,Umasikini
unaendana na udhalilishaji na Ujinga na Maradhi,ni mwana Siasa pekee
ambae hasifiii umasikini kwani ni vita katika vita kuu za taifa hili
tangu tunapata uhuru. Hii imekuwa hulka ya viongozi kadhaa hasa wabunge
wetu hutuhadaa wakisema tuwape ridhaa ya kutuongoza kwa sababu wao ni
masikini wenzetu, siasa sasa ya leo na kimataifa imebadilika mno
tukiangalia mataifa makubwa hata madogo , viongozi ni wale wenye majibu
sahihi katika kuufuta umasikini na si kujisifia kuwa wewe ni masikini
tukupe ridhaa tena ridhaa ambayo utahakikisha kujinufaisha wewe na famia
yako kwanza, na CCM sasa inataka kujenga uchumi imara uchumi ambao
utafuta umasikini kwa kumpa Mtanzania Elimu, kuimarisha miundombinu na
kufungua biashara tujifunze haya toka Kenya waungwana.Pia ni miongoni
mwa sababu zinazo wavutia wana CCM kumpa ridhaa ya kupeperusha bendera.
4.ANAPENDWA NA WATANZANIA WOTE NA WANAMUHITAJI
Ni
mtu ambaye ana mvuto mkubwa kwa watanzania na ana sifa ya kuwa
muadilifu, mtendaji mzuri, mbunifu, huheshimu mawazo ya wengine, anaijua
Tanzania, Mfuatiliaji wa kazi, anatabia ya kuwapa watu matumaini
Mpambanaji (fighter) na anaheshimika kikanda na kimataifa. Ni Mtanzania
pekee anayependwa na kukubalika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndani
na nje ya chama chake. Ni mtu ambaye ana Aura ya aina yake na huleta
matumaini unapokaa naye na kusikiliza.Ni kweli kabisa..Edward Lowassa
(is the chosen one) kaatika uhai wa siasa ya chama chochote inatakiwa
kuwa na gombea anaye uzika, anayekubalika na ambaye ni tumaini la
mahitaji wananchi husika, Lowassa amekidhi vigezo vyote na hakika anafaa
ndani ya CCM na ndio chaguo sahihi kama chama kinahitaji uhai wa muda
mrefu.
5.KIONGOZI ALIYEPITIA MENGI NA ANAYEIJUA NCHI.
Lowassa
ni kiongozi alie pitia mengi kama rais wa awamu ya pili alhajj Ali
Hassan Mwinyi kufikia hatua ya kujiuzulu na kuwajibika kama kiongozi
ambaye anjua fika maadili ya kiongozi wa umma, Lowassa amengia katika
mfumo wa chama na serikali tangu mwaka 1977 ambapo imepita miaka Zaidi
ya 30 akipambana na shida na mahitaji ya watanzania, mwenyekujua nini
Watanzania wanahitaji, mtu ambaye amepitia mengi na kuwa na ufahamu wa
kutosha wa serikali na chama chake kiasi cha kufanya kuwa kiongozi pekee
kwa sasa anayekijua chama na serikali. Chama cha Mapinduzi kimekosa mtu
mwenye sifa hizi mtu ambaye amepitia mikiki mikiki ya kina katika
kuwatetea wananchi, kiongozi ambaye amepambana mpaka na mahafidhina
ndani ya chama na kiongozi ambae si rahisi kumpelekesha, kiongozi huyu
ameweza kuwa adui mkubwa wa mahafidhina kwa sababu hana si ya woga dhidi
yao, hawafumbii macho na naweza sema huyu ni kama TAKUKURU kwa
mahafidhina sababu hafumbii macho machafu.
MWISHO.
Watanzania
tunahitaji kiongozi ambae atakuwa mrithi sahihi wa serikali ya awamu ya
tatu, mtu ambae atatuongoza katika kukabiliana na mahitaji yetu yaani
nini watu wa namanyere, uvinza nantumbo na Tanzania kwa ujumla nini
wanataka, Mtu ambaye atakuwa msikivu na mpambanaji wa mahitaji yetu ,
nashauri wote kwa pamoja tuwajadili watu wanaoweza kuiongoza nchi yetu
bila kejeli, matusi au woga na aina yeyote ya kufumbia macho machafu ,
kuukuza uzalendo ni pamoja na kuukana woga wa kivuli chako. MUNGU
IBARIKI TANZANIATOA MAONI YAKO HAPA CHINI
