CCM YABOMOA JENGO LA TANU JIJINI DAR ES SALAAM
JENGO
la ofisi ndogo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Lumumba Dar
es Salaam ambako ndiko kilizaliwa Chama cha Tanu limebomolewa ili
kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho.
Akizungumza Dar
es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema
jengo hilo limebomolewa kwa ajili ya matengenezo ya kawaida.
"Tunachokifanya
katika jengo hili ni ukarabati wa kawaida,"alisema Nape wakati
akielezea jengo hilo ambalo limebomolewa jana kwa kutumia tingatinga.
Kutokana
na kubolewa kwa jengo hilo , viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrhaman Kinana , watakuwa katika Jengo la Umoja
wa Vijana wa chama lililopo barabara ya Morogoro, wakati ukarabati wa
jengo hilo lililobomolewa ukiendelea.
Awali baadhi
ya makada wa chama hicho waliokuwa eneo hilo, walidai kuwa jengo hilo
la Tanu limebolewa ili kupisha ujenzi wa jengo la kisasa ambalo
litatumika kwa ajili ya kitega uchumi.
Makada hao walisema jengo hilo litakapokamilika litakuwa la kisasa zaidi tofauti na jengo ambalo lilikuwepo eneo hilo.