Ang’atwa na Nyoka Akizini na Mke wa Mtu Kichakani
Kijana
mmoja shija kasamwa mwenye umri wa miaka 28,leo mchana amejikuta
akipata masahibu ambayo iwapo atapona kamwe hatayasahau kabisa ktk
maisha yake.
Kijana
huyo mkazi wa mkoa wa Shinyanga ktk kijiji cha Chela ameng’atwa na
nyoka mwenye sumu kali akiwa msituni akivunja amri ya sita na mke wa
mtu.
Inasemekana ndio ilikuwa tabia yake kufanya uchafu huo na mwanamke huyo asiye mwaminifu ktk ndoa yake.
Sasa
leo kama kawaida yao walijirusha msituni,wakiwa huko kabla hawajaanza
kufanya mapenzi walisikia sauti za watu wakija upande waliokuwepo ndipo
wakaamua kuingia kichakani kwa hofu ya kuonekana,ndani ya kile kichaka
kikubwa kilichokuwa kimefungasha miti mingi kiasi kwamba haikuwa rahisi
kuonekana kwao,ndipo wakaamua kufanya uchafu wao eneo hilo ndipo wakiwa
bado wanaendelea na starehe ilihali yule kijana akiwa kashusha suruali
yake na makalio yake kubaki wazi alishtuka ghafla kang’atwa na nyoka
huyo anayesadikiwa kuwa ni aina ya cobra,kelele za maumivu zikakusanya
wanakijiji na mke wa mtu akakimbia kwa hofu.
