Waziri muhongo azomewa na wananchi wa soko la wakulima kahama
Waziri
wa nishati na madini Mhe.Sospeter Muhongo amejikuta katika wakati
mgumu na msafara wake baada ya kuzomewa na wananchi wa soko la wakulima
katikati ya mji wa Kahama wakati akitokea kwenye ziara yake vijijini
wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio
hilo limetokea hivi karibuni wakati waziri huyo na msafara wake
wakitokea kata ya Bulungwa kwenye jimbo la Kahama kuelekea kata ya
Bulige jimbo la Msalala kukagua ujenzi wa mradi wa umeme vijijini
unaotekelezwa na wakala wa umeme vijini nchini (REA) unaoendelea
kufungwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Baada
ya kufika katika eneo hilo wananchi hao walianza kumzomea wakidai ni
“mwizi wa fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kelele
ambazo ziliwashtua watu wengi ambao walijitokeza kuona anayezomewa ni
waziri yupi.
Hata
hivyo kelele hizo ziliisha baada ya msafara wa waziri huyo ambaye yuko
ziara kanda ya ziwa kutokomea na kuacha makundi mbalimbali katika eneo
hilo la soko la wakulima wakijadili hatima yake katika mpango mzima wa
mgogoro wa uchotwaji wa mabililioni ya shilingi kwenye akaunti hiyo ya
Escrow.
Pamoja
na kuzomewa na wananchi hao Muhongo katika ziara yake wilayani Kahama
ameacha neema kwa wananchi wa halmashauri ya Ushetu baada ya kuwaahidi
umeme katika awamu ya tatu ya mradi ya nishati vijijini.