WANAFUNZI 84 WA UDOM MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHAMASIHA MAANDAMANO MKOANI DODOMA
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 84 wa chuo Kikuu UDOM
kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni na kufanya maandamano
haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa
Serikali zilizopo Dodoma Mjini leo tarehe 14.01.2015 majira ya 05:30hrs.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – (SACP) ameeleza kuwa chanzo cha wananfunzi hao wa programu
maalum ya Diploma ya Ualimu kufanya uhalifu huo ni kikao walichofanya
wananfunzi hao tarehe 13.01.201 wakidai kuongezewa posho ya chakula na
kwamba hata kiasi ambacho wanapewa wamechelewa kupewa.
Hata
hivyo uongozi wa Chuo uliwaeleza kuwa wenye mamlaka ya kuzungumzia
swala la kuongezewa posho ni Bodi ya Mikopo na siyo chuo. Hivyo
walitakiwa kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao. Pia walielezwa
kuwa hundi kwa ajili ya fedha za posho zao zimeshasainiwa na
kuwasilishwa Benki ili waweze kuanza kupewa posho zao.
Wanafunzi
hao hawakuridhika na usiku wakaanza kuhamasishana kufanya maandamano
jambo ambalo ni kosa kisheria. Wanafunzi hao wamehojiwa kulingana na
ushahidi ambao umekusanywa na wamefikishwa mahakamani kwa kosa la
Kufanya Maandamano yasiyo na kibali. Viongozi waliohamasisha uvunjifu
huo wa sheria baadi wamekamatwa na baadhi wanaendelea kutafutwa ili nao
waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Ushahidi uliokusanywa unaonyesha jinsi
viongozi hao wameshiriki kuhamasisha kupitia vikao rasmi na visivyo
rasmi, katika vikundi, kupita katika mabweni na kutuma sms.
Kamanda
MISIME ametoa wito kwa Wanafunzi hao kutumia taratibu zilizowekwa na
Serikali na Chuo kuwasilisha malalamiko yao ngazi kwa ngazi na siyo
kufanya vitendo vya kuvunja sheria ambavyo vitawasababishia kukamatwa.
Endapo watafanya hivyo wasije kulaumu mtu kwani hatua zitachukuliwa
kulingana na Sheria inavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kufikishwa
mahakamani.
Baadhi
ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa chini ya ulinzi
kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya
maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za
viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.
Baadhi
ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa kwenye gari ya
polisi baada ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa
amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea
katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma
leo.
.jpg)
.jpg)