UNYAMA..............WATU WATATU WAPIGWA, WAUAWA NA KISHA KUCHOMWA MOTO
Wakazi wa Nzega, Tabora wamewapiga, kuwaua na kuwachoma moto watu watatu kwa tuhuma za kushiriki kumuua Helena Abel na kumjeruhi mume wake, Said Msoma.
Kamanda
wa Polisi Tabora, Juma Bwile amethibitisha kuokea kwa tukio hilo ambapo
Helena Abel na mume wake Said Msoma walivamiwa katika tukio hilo,
Helena aliuawa na Said Msoma alifanikiwa kumjeruhi mmoja wa wahalifu hao
ambaye alikimbia.
Kamanda Juma amesema wananchi walifanya doria na kumkamata mhalifu huyo aliyejeruhiwa ambaye anaitwa Mainda Mahila na kuanza kumhoji kuhusika na mauaji hayo na kukiri kufanya hivyo.
Bwile alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliwaeleza wananchi hao kuwa mauaji hayo alifanya kwa kuagizwa na Mama Zainabu Hamis pamoja na mtoto wake, Zena Yasoda ambapo wananchi hao waliwapata watuhumiwa wote wawili kisha kuanza kuwapiga hadi kufa na baadaye kuwachoma moto.
Wakati huohuo mtu mmoja Chenge Kasinki alivamiwa na kuuawa nyumbani kwake na watu wasiofahamika
