UFAFANUZI KUHUSU PICHA ZA PANYA ROAD ZILIZO SAMBAA MITANDAOINI HUU HAPA
Moja ya story ambazo zimechukua
headlines siku ya leo ni ishu ya watu kadhaa kulalamikia kwamba picha
zao zimeonekana kwamba wao ni watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa kujihusisha
na kundi la Panya Road.
Leo katika kipindi cha XXL ya Clouds FM, Kamanda wa Polisi Suleiman Kova ameongelea story hiyo; “Kuna
mtu aliniuliza swali siku ya leo, mimi mwenyewe nilitoa picha tatu
kwamba hao ndio realy leaders ile ya Press Conference tuliyofanya, baada
ya hapo sijatoa tena picha nyingine, isipokuwa ninachofahamu mimi ni
kwamba badae nikaona kwenye gazeti hilo kuna picha yangu mimi ambayo
sikupigwa siku hiyo au jana yake nikaona kuna picha nyingine, zote ni za zamani hizo.
Sasa
inawezekana mle ndani huyo kijana yumo lakini jibu ni kwamba hiyo ni
kazi ya waandishi wa habari… yani ninyi huwa mna taratibu zenu kwamba
likitokea tukio fulani labda liwe la michezo au la vita mnachukua
background picha ambazo zipo unaona sasa mimi tena siwezi kulaumiwa
kwamba eti hizo picha zinanihusu mimi, mbona hata mimi ya kwangu ilitoka
nikiwa na cheo cha Senior Assistant Commissioner… lakini nimekubali tu
kwa sababu najua cha muhimu pale ni message kwa wananchi kwamba kuna
suala la panya road na hata kuna wengine walishakamatwa siku za nyuma.
Kwa
hiyo sisi Polisi hatuwezi kuendelea kulaumiwa kwamba kwa nini hizo picha
zimeonekana… sie hatujazipeleka, tulizozipeleka ni tatu tu ambazo hao
watu hawajalalamika, kwa hiyo kama wakitaka huyo bwana aulizwe kwanini
wamemchapisha kwanza nyinyi sasa ndio mnatakiwa muwaeleweshe hawa raia
kwamba hizo picha ni kawaida yetu sisi huwa tunazitoa hivyo ilimradi ni
ishu ambazo zina mahusiano, unakuta mmetoa picha za Rais za miaka mitatu
iliyopita au Waziri… au mtu yoyote yule unatoa kwani ukitoa zile
atasema mbona sijapigwa picha?“– Suleiman Kova.