SHEIKH PONDA ARUDISHWA LUMANDE
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro leo imemnyima dhamana Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa katika kesi
yake inayomkabili ya jinai namba 128 ya mwaka 2013.
Kesi
hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Marry Moyo ambaye amesema
amepokea hati ya kumfutia dhamana Sheikh Ponda kutoka kwa Mkurugenzi wa
Mashitaka nchini (DPP) kwa mamlaka aliyonayo hivyo yeye hana mamlaka ya
kuikataa hati hiyo.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Januari 26 na 27, mwaka huu itakaposikilizwa tena.