SHARE UJUMBE HUU KUPINGA KUTUPWA KWA WATOTO WACHANGA, MASIKINI KICHANGA CHA UAWA NA KUTUPWA HAPA
Mwili wa kitoto kichanga uliotupwa kwenye jalala.
Stori: Mwandishi Wetu, Mbeya/UWAZI UKATILI,
Mtoto mchanga ambaye anasadikika kuwa wa siku saba, amekutwa akiwa
ameuawa na mwili wake kuwekwa kwenye mfuko wa rambo kisha kutupwa
pembeni mwa jalala. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Mtaa wa
Kaloleni katika Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya .
Wakizungumza
na gazeti hili mashuhuda ambao hawakupenda majina yao kuandikwa
gazetini walisema kuwa walimkuta mtoto huyo akiwa amenyongwa kisha
kuwekwa kwenye karatasi ya naironi (rambo) .
Waliongeza
kuwa mtoto huyo alitambulika baada ya watoto wadogo wakiwa katika
michezo yao katika maeneo yao kuuona mfuko huo wa rambo na kuufungua
ndipo wakatoa taarifa wa wazazi wao,” alisema mmoja wa wazazi wa eneo
hilo.
“Hiki
kitendo ni kibaya sana na aliyefanya unyama huu anastahili adhabu
kali. Huwezi kulea mimba miezi tisa kisha unamza mtoto na kumnyonga
shingo hadi kufa, ni ukatili uliokithiri, tena mtoto huyu ni kama wa
siku saba, hii ni kwa sababu kitovu chake kilionesha dalili za kupona,”
aliongeza.
Hata hivyo, aliyefanya kitendo hicho cha kikatili
hakuweza kutambulika mara moja.
Wakithibitisha habari hiyo, kiongozi mmoja wa polisi katika kituo kidogo cha Tunduma alisema ni kweli kimetokea na mwili huo wa mtoto huyo umepelekwa katika hospitali ya serikali iliyopo mjini hapa kwa ajili ya uchunguzi.
hakuweza kutambulika mara moja.
Wakithibitisha habari hiyo, kiongozi mmoja wa polisi katika kituo kidogo cha Tunduma alisema ni kweli kimetokea na mwili huo wa mtoto huyo umepelekwa katika hospitali ya serikali iliyopo mjini hapa kwa ajili ya uchunguzi.
“Tunaomba
wenye kujua aliyefanya haya atuletee jina ili tumkamate,” alisema
ofisa huyo bila kutaja jina lake kwa kuwa siyo msemaji wa polisi.
Msemaji wa jeshi hilo mkoani Mbeya ni SACP Ahmed Msangi (pichani).
