SHARE HABARI HII ILI KUONESHA UPENDO KWA WATOTO: MAMA AMCHARANGA VIWEMBE VYA USONI MWANAYE
Unyama wa kutisha! Mama mzazi
aliyetajwa kwa jina la Feromena, mkazi wa Meko-Mtongani, Kunduchi
jijini Dar, anatuhumiwa kumcharanga viwembe mwanaye wa kumzaa
aliyetajwa kwa jina moja la Zena mwenye umri wa miaka kumi.
Mtoto anayefahamika kwa jina la Zena anayedai kunyanyaswa na mama yake.
Tukio
hilo la kulaaniwa lilijiri Jumanne wiki hii nyumbani kwa mwanamke huyo
maeneo hayo ambapo mama huyo inadaiwa alimsulubu mwanaye huyo
anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Mtakuja.
Sehemu ya majeraha ya viwembe kichwani kwa mtoto Zena.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mama huyo alidaiwa kumfungia ndani
mwanaye huyo na kuanza kumpa kipigo cha mbwa mwizi.Walidai kwamba
ukiachana na siku hiyo, mama huyo amekuwa akimsulubu mwanaye huyo mara
kwa mara kwa kumcharanga viwembe na vitu vyenye ncha kali hivyo
kumwachia majeraha sehemu mbalimbali za mwili.
Sehemu ya majeraha yaliyo mgongoni mwa zena.
Mjumbe
wa mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Mziga alikiri
kupokea malalamiko kutoka kwa majirani juu ya unyanyasaji na uteswaji
wa mtoto Zena.Mjumbe huyo alisema kuwa tuhuma hizo alishazifikisha
polisi ambapo mama huyo alikamatwa lakini baada ya muda alionekana
akidunda mtaani kama kawa.
Mama mzazi wa mtoto Zena,Bi.Feromena akibanwa kwa maswali.
Baada
kujazwa habari na majirani na mjumbe huyo, kile kikosi kazi cha
Oparesheni Fichua Maovu cha Global Publishers kiliingia mzigoni ambapo
kilianza kwa kumsaka mtoto huyo na kuzungumza naye.
Alipopatikana, mtoto Zena alieleza namna mama yake alivyokuwa akimfanyia matendo ya kinyama huku akimnyima haki ya msingi ya kwenda shule.
Alipopatikana, mtoto Zena alieleza namna mama yake alivyokuwa akimfanyia matendo ya kinyama huku akimnyima haki ya msingi ya kwenda shule.
Mama Zena, Bi. Feromena akiwa chini ya ulinzi.
Alisema
mama yake amekuwa akimtuhumu kumwibia fedha zake na kwenda kutumia
shuleni hivyo hakupaswa kurudi tena shuleni na kuongeza kuwa siku
ambazo alikuwa akilala kwa amani ni zile ambazo alikuwa ametoroka
nyumbani na kwenda kulala kwa majirani.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo wa kusikitisha.
OFM
ilishuhudia mwili wa Zena ukiwa na makovu na kuvimba huku akidai kuwa
aliunguzwa na ‘frampeni’ (kikaangio) hasa sehemu za kiunoni na
mgongoni.Alisema mama yake alimtishia kuwa endapo atamwambia baba yake
atakiona cha mtema kuni.
“Jamani
mama amekuwa akinipiga na kunikata viwembe bila kuniambia kosa langu.
Naombeni msaada nateseka,” alisema Zena kwa masikitiko makubwa.OFM, kwa
kwa kushirikiana na mjumbe wa eneo hilo walikwenda kuripoti tukio hilo
kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mtongani lakini hakukuwa na dawati
la jinsia hivyo polisi walikwenda kumkamata mama huyo kwa ajili ya
kumpeleka kituo kikubwa.
Moja ya wazee akionesha jalada la kesi aliyofunguliwa mama zena.
Kwa
upande wake mama huyo alipoulizwa sababu hasa ya kumsulubu mwanaye
alisema si kweli bali anachojua ni siku moja aliyompiga baada ya
kuchukua fedha zake na kwenda kununulia maandazi.
“Sijui aliyemkatakata viwembe,” alisema mama Zena kwa kifupi.
“Sijui aliyemkatakata viwembe,” alisema mama Zena kwa kifupi.
Baada
ya kufikishwa kwenye kituo kikubwa cha Polisi cha Kawe, mama huyo
alifunguliwa jalada la kesi namba KW/RB/439/015-SHAMBULIO LA KUDHURU
MWILI hivyo anasubiri kufikishwa kwenye mkono wa sheria.