RONALDO KURUDI MAN U SASA
Christiano Ronaldo akisherehekea bao lake dhidi ya Barcelona
Aliyekuwa
msaidizi wa kocha wa Manchester united Mike Phelan anaamini kuwa
Cristiano Ronaldo huenda akaandikisha mkataba wa kurudi katika kilabu ya
Old Trafford katika siku sijazo.
Ronaldo
amehusishwa na mpango wa kurudi Manchester United katika muda wake
katika kilabu ya Real Madrid ,lakini mpango kama huo haujazaa matunda
kufikia sasa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye
alichezea
Man U anafurahia maisha yake katika kilabu ya Real Madrid lakini Phelan
anaamini huenda akashawishika kurudi katika ligi ya Uingereza.CHANZO
BBC