RIPOTI KAMILI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KUJULIKANA KESHO.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM,Ndugu Adam Kimbisa,wakati akitoka nje mara baada ya kumaliza kikao
cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa usiku huu,kilichofanyika leo
katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja,Zanzibar,kikao hicho
kilianza mnamo majira ya saa sita mchana na kumalizika usiku mnamo saa
mbili na ushehe hivi huku mambo mbalimbali yakiwa yamejadiliwa ikiwemo
suala la sakata la Akaunti ya Escrow,Hali ya kisiasa nchini,uchaguzi
Mkuu na mambo ya Maadili na mengineyo.
Pichani
ni Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na
Wanahabari usiku huu baada ya kikao cha kamati kuu cha CCM kuisha nje ya
ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani
Zanzibar.Nape ameeleza kuwa taarifa rasmi ya yaliyohusu kikao hicho
atayaweka wazi mapema kesho asubuhi.

