RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WAJUMBE WA JOPO LA KUTATHMINI PROGRAMU YA TEKELEZA KWA MATOKEO MAKUBWA SASA (BRN)
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Ijumaa, Januari 16, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na
wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea Iliyofanya Tathmini ya
Utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Katika mazungumzo
hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam
Rais
Kikwete amewashukuru wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea iliyofanya
tathmini ya utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais
Kikwete amewashukuru kwa kazi nzuri wajumbe hao saba wa Kamati hiyo ya
BRN Independent Review Panel ikiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana,
Mheshimiwa Festus Mogae. Wajumbe
Wajumbe
wengine wa Kamati hiyo ni pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Benki
ya Dunia Dkt. James Adams, aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Bwana
Tony Blair ya Uingereza Lord Mandelson, Gavana wa Benki Kuu ya Botswana
Bi. Linah Mohohlo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya ONE Bi. Sipho Moyo.
Wengine ni Bwana Knut Kjaer kutoka Norway na Bwana Nkosana Moyo.
Wajumbe
hao wamekutana kwa siku mbili kuanzisha Alhamisi, Januari 15, 2015
mjini Dar es Salaam ambako wametathmini mwaka wa kwanza wa utendaji wa
BRN baada ya kuwa wamepokea maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa
Presidential Delivery Bureau (PDB), mawaziri sita ambao wanaongoza sekta
ambazo ziko katika BRN kwa sasa na timu maalum ya Kampuni ya PWC ambayo
ilifanya ukaguzi matokeo ya utendaji ya mwaka wa kwanza wa BRN.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam.
16 Januari,2015
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na wajumbe wa Jopo la
Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN
Independent Review Panel) linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana
Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae ( aliyekaa wa kwanza kulia kwa Rais
Kikwete) huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Results
Now kwa Rais Mstaafu wa Botswana Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae
aliyeongoza jopo maalum la kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo
Makubwa Sasa huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Result
Now kwa Dkt. Sipho Moyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ONE wa Kanda ya Afrika
aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa jopo la kutathmini Programu ya
Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa. Rais Kikwete aliwakabidhi tuzo hizo
huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi Tuzo Maalum ya Vision 2025 Big Results
Now kwa Bwana James Adams, Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia
aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya
Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal
wakipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya
Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN Independent Review Panel). Kulia
kwa Mheshimiwa Rais Kikwete ni Rais Mstaafu wa Botswana Dkt. Festus
Mogae akifuatiwa na Bwana James Adams (Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki
ya Dunia), aliyesimama wa kwanza kushoto ni Bibi Linah Mohohlo (Gavana
wa Benki Kuu ya Botswana) na wa kwanza kulia ni Dkt. Sipho Moyo
(Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika, ONE. Waliosimama mstari wa
nyuma (kulia kwenda kushoto) Dkt. Nkosana Moyo (Mwanzilishi wa Mandela
Institute for Development Studies) akifuatiwa na Lord Peter Mandelson
(Mwenyekiti, Global Counsel ‘Uingereza’), anayefuata ni Bwana Knut
Kjaer, (Mwenyekiti, Trident Asset Management, ‘Norway’) PICHA NA JOHN
LUKUWI
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)