MTOTO WA RAILA ODINGA AFARIKI DUNIA
MTOTO
wa kwanza wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Fidel Odinga
amefariki dunia leo alfajiri akiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika. Raila Odinga amethibitisha
kifo hicho.
Fidel
alikimbizwa hospitali na mkewe baada ya kuwasili nyumbani majira ya saa
7 usiku wa kuamkia leo na kulalamika kuwa anapata shida katika
upumuaji.
Fidel
na baba yake Raila, jana mchana walipata chakula cha mchana pamoja na
kiongozi huyo wa Cord ameeleza leo asubuhi kuwa kijana wake hakusema
kama ana tatizo lolote la kiafya. Baadaye jioni marehemu alitoka na
marafiki zake ambapo alirejea nyumbani saa 7 usiku na kudai kusumbuliwa
na tatizo la upumuaji.