MCHEPUKO AGOMBANIA MTOTO NA MWENYE FAMILIA
Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Makubwa! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke wa mtu aliyekuwa akiishi ukweni na mumewe wa ndoa, Bahati Ramadhani, amenusurika kuuawa na ndugu wa mumewe wakiwemo mawifi na wakwe zake baada ya kudaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko wake na kujikuta wakigombea mtoto.

Mwanamke, Bahati Ramadhani akiwa chini ya ulinzi wa Polisi. |
Tukio
hilo la kushangaza lililojaza kadamnasi lilijiri nyumbani kwa wakwe
hao, Mtaa wa Mawenzi jirani na Soko la Matunda la Mawenzi la mjini hapa
wiki iliyopita ambapo Bahati alikuwa akiishi na mumewe, ldd Yusuf.
Ilielezwa kwamba wanandoa hao walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume (jina kapuni) ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 2.
Siku
ya tukio, mama mkwe wa Bahati, Faidha Cosmas alishtukia dili baada ya
kuona sms ya mwanaume ‘aliyeseviwa’ kwa jina la Saddy kwenye simu ya
Bahati ikimweleza kwamba alikuwa amemtumia fedha za matumizi ya mtoto
wao huyo.
Baada
ya mama mkwe kuona ishu hiyo alimwambia mwanaye Idd ambapo kwa pamoja
walimpigia Saddy aliyekiri kuwa anachojua mtoto huyo ni wake na amekuwa
akituma fedha za matumizi.
Mama mkwe alisema kwamba walimwita Bahati na kumuuliza kama anamfahamu Saddy ambapo alikiri kuchepuka.
Mama mkwe alisema kwamba walimwita Bahati na kumuuliza kama anamfahamu Saddy ambapo alikiri kuchepuka.
Baada
ya mzozo wa hapa na pale, mawifi wa Bahati waliingilia kati na kuibua
bonge la mtiti wakimpa wifi yao kipigo hadi mwandishi wetu alipotonywa
na kufika eneo la tukio.
Alipofika mahali hapo na kuona hali ya hatari ndipo akaita polisi wa doria ambao walifika na kutuliza ghasia.
Alipofika mahali hapo na kuona hali ya hatari ndipo akaita polisi wa doria ambao walifika na kutuliza ghasia.
Familia hiyo ilishuhudiwa ikiwa kwenye kikao ambapo uamuzi wa awali ulikuwa ni ldd kumuacha mara moja Bahati.
Hata
hivyo, katika uamuzi huo wa awali, Bahati alikubali kuondoka lakini kwa
masharti ya kuondoka na mwanaye jambo ambalo liliikera familia hiyo na
kumvamia wakitishia kumtoa roho.
Kabla ya mambo kuwa mabaya, polisi wakiongozwa na Afande Mwajabu waliingilia kati na kumuokoa Bahati.
Kabla ya mambo kuwa mabaya, polisi wakiongozwa na Afande Mwajabu waliingilia kati na kumuokoa Bahati.
Afande
Mwajabu aliwahoji wahusika na baada ya maelezo, ldd alitoa uthibitisho
wa kadi ya kliniki ambayo ilionesha yeye ndiye baba halali wa mtoto
huyo.
Katikati ni mtoto anayegombewa katika utata uliojitokeza.
Mwandishi
wetu pamoja na Afande Mwajabu walimpigia simu Saddy ambaye kwa sasa
yuko masomoni mkoani lringa na kuweka ‘loud speaker’ ambapo alipoulizwa
alisema:
“Mtoto ni wangu. Kwa sasa ana umri wa miaka 2 na kadi ya kliniki ninayo.”
Saddy alipoulizwa na mwandishi wetu kwa kipindi chote cha miaka miwili, mtoto wake alikuwa akiishi wapi alisema:
Saddy alipoulizwa na mwandishi wetu kwa kipindi chote cha miaka miwili, mtoto wake alikuwa akiishi wapi alisema:
“Nilikuwa bize na masomo lakini najua mwanangu yuko na mama yake.”
Kwa upande wake, Idd ambaye ndiye anayeishi na Bahati (huku akitokwa machozi) alisema hakutarajia kama mkewe angemsaliti kiasi hicho.
Bahati alipohojiwa, alisema kuwa siku aliyopata ujauzito alitembea na Saddy pamoja na mumewe ldd hivyo hata yeye anashindwa kujua baba halali wa mtoto wake.
Sakata hilo lilifikishwa polisi ambapo bado linatafutiwa suluhu.