HUYU NDIYE BINTI MDOGO ZAIDI KUTOKA AFRIKA ALIYEVUNJWA REKODI YA AJABU
Unapokuwa
karibu na mtoto wako na kumfuatilia ni rahisi kujua kipaji chake na
kukiendeleza ingawa ni wazazi wachache wanaoweza kufanya hivyo, msichana
kutoka Nigeria ambaye anasoma Marekani anakuwa msichana mdogo
aliyeweza kuvunja rekodi kadhaa kubwa duniani.
Zuriel Oduwole, umri wake ni miaka 12, ameweka historia nyingine baada ya documentary yake ya ‘A Promising Africa’ kuwa documentary ya binti mdogo zaidi duniani kuonyeshwa katika majumba makubwa ya cinema.
Jarida la Forbes
lilimtaja kuwa msichana mdogo mwenye asili ya Afrika ambaye ni
miongoni mwa watu 100 mashuhuri wenye ushawishi zaidi Afrika waliotajwa
kwa mwaka 2013 wakiwemo Marais watatu, pia akawa na rekodi ya kuwa mtu
mdogo zaidi dunia kuandikwa historia yake katika Jarida la Forbes.
Documentary hiyo itaonyeshwa London, Januari mwaka huu na baadaye itaanza kuuzwa.