Dk.Bilal kuweka jiwe la Msingi Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB)
MAKAMU
wa Rais ,Dk.Mohammed Gharib Bilal anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika
sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB),
zitakazofanyika Jumamosi Januari 17 katika Kijiji cha Kiromo, Bagamoyo
Mkoani Pwani.
Akizungumza
na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam, Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Fedha na Utawala,
Dk.Elifuraha Mtalo alisema sherehe hizo zitafanyika Katika Kijiji cha
Kiromo na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa
Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao unatarajiwa kuanza
Mwaka huu.
Dk.Mtalo
alisema Dk.Bilal ndiye atakuwa mgeni rasmi pia na Rais Mstaafu
Benjamin Mkapa naye anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni walioalikwa
katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu
Somo la Historia linatufundisha kuwa mji wa Bagamoyo watumwa walikuwa
wakiishi.
"
UB tunaifahamu historia ya Mji wa Bagamoyo ndiyo maana tukaamua
kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la University of
Bagamoyo.Kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, hivyo kupitia UB
ambayo inajenga makazi yake ya kudumu katika mji huo, binadamu wote
watakuwa huru kwasababu tutapata elimu" alisema Dk.Mtalo.
Alisema
UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya
muda ,Mikocheni B, Dar es Salaam na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu
ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa
eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu na
ajira.
Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo
