DAR YA CHAFUKA USIKU HUU PANYA ROAD KILA KONA YA JIJI WATU WAJIFUNGIA NDANI
Hali ya kuogopesha imetanda katika maeneo ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ya Sinza,
Kinondoni, Mwananyamala, Mabibo, Magomeni, Manzese, Kagera na
Mburahati usiku huu,kwa kile kinachoelezwa kuwa kuna kundi la vijana
waitwao Panya Road wamevamia maeneo hayo na kuingia kwenye baadhi ya
maduka kwa lengo la kuiba na kuwajeruhi watu kwa vitu vyenye ncha kali
(visu na mapanga) walivyokuwa navyo.
hali
si shwari katika maeneo mengi hapa jiji la Dar,maana watu wanakimbia
hovyo barabarani kwa kuwakwepa Panya Road hao ambao wamechafua kabisa
hali ya hewa hapa mjini.
Maduka
mengi ambayo siku zote hufanya biashara mpaka usiku wa kati,leo hii
yamefungwa mapema kwa kuhofia kudhuriwa na Panya Road.
Chanzo
chetu cha habari kinaeleza kuwa vijana hao waitwao Panya Road wameibuka
na kufanya uhalifu huo mara baada ya tukio la Mwenzao mmoja kudaiwa
kuuwawa na Polisi.Aidha Chanzo hicho kimebainisha kuwa baada ya taarifa
kusambaa kwa haraka,kimeeleza kuwa Jeshi la Polisi limeingia kazini
kuwasaka watuhumiwa hao walioibua tafrani kubwa usiku huu.
Wadau tutazidi kuwaletea taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana.