ATOBOLEWA MACHO BAADA YA KUTOKA NA MKE WA MCHEZA KARATE
AIBUUU....NJEMBA NUSURA ITOLEWE JICHO BAADA YA KUCHEPUKA NA MKE WA MCHEZA KARETI
Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini
Dar es Salaam, Nuru Makala 'BabaEliza' (42) Jumatano iliyopita
alikumbwa na majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina
la Yusuf Ally 'Mgosi wa Ndima' kudai amemfumania Baba Eliza
akiwa na mkewe ambaye jina halikupatikana.
Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka
huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
Akizungumzia tukio hilo mbele ya wanahabari waliokuwa eneo
hilo wakisaka habari, Yusuf Ally ambaye ni mume wa mwanamke
aliyefumaniwa alisema:
"Nilikuwa katika
harakati za kumchunguza mke wangu kinyemela kwa siku nyingi
kama anachepuka, nikabaini kuna mawasiliano yenye shaka kati
yake na huyo jirani yangu.
"Nilipomuuliza mke
wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba
haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane, tena
wakutane humu ndani.
"Ndipo nilipoamua kumuandaa mke
wangu kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku ya tukio)
sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi.
Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa
sungusungu wa eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea
kinagaubaga