ASKARI TANZANIA WAONGOZA KWA WIZI WA WAZI
Idara
ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania
kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Ripoti
hiyo inasema kuwa maafisa wa polisi walipokea asilimia 25 ya hongo zote
zilizotolewa kwa wafanyikazi wa taasisi za uma mwaka uliopita.
Ya
pili ni idara ya mahakama,ambayo wafanyikazi wake walitia mfukoni
asilimia 18 ya hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya usajili na
utoaji wa leseni yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.
kwa
mujibu wa gazeti la The Citizen, Idara ya Polisi nchini Tanzania
imetajwa kuwa ya tatu kwa ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne.
Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki.
Utafiti
huo ulifanywa mwezi Julai na Agosti mwaka uliopita na shirika la lenye
na maslahi ya kimaendeleo barani afrika ForDIA likishirikiana na Jukwaa
la uwazi nchini tanzania Trafo.
Vipi mdau una maoni yoyote kuhusiana na ripoti hii???
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI USIKIKE !