ALIYEOMBA KUSAIDIWA KUFA AKATALIWA
Nchi ya Ubelgiji ilipitisha sheria ya watu wanaotaka kufa kusaidiwa kwa kudungwa sindano kwa miaka 12 iliyopita.
Frank Van den Bleeken aliwasilisha
ombi lake kwa Serikali ya nchi hiyo kwamba asaidiwe kufa kwa kudungwa
sindano yenye sumu ili kumwepushia msongo wa mawazo anaokabiliwa nao
kutokana na kukabiliwa na kesi ya mauaji na ubakaji.
Wizara ya Sheria Ubelgiji kupitia kwa Waziri wake Koen Geens amesema anaheshimu ushauri wa madaktari wanaomtibu mtuhumiwa huyo aliyeiomba Serikali kumsaidia kifo chake.
Kwa miaka mingi mtuhumiwa huyo alisema
kuwa alishindwa kabisa kubadili au kukomesha tabia yake ya ubakaji na
kutokana na hilo haoni uwezekano wowote wa kuachiwa huru hivyo aliomba
kuchomwa sindano ili apoteze maisha.