SIRI YA KAGERA SUGAR KWA SIMBA HII HAPA

Burudani ya ligi kuu ya Tanzania bara inayodhaminiwa na vodacom inataraji kuendelea leo kwa mchezo mmoja katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha simba sc na Kagera sugar.

Mchezo wa mwisho wa ligi kwa simba sc waliibuka na ushindi dhidi ya ruvu shooting baada ya kutoa sare michezo 6 kabla ya kuwa vaa ruvu. Wakati Kagera sugar wanaingia katika mchezo huo wakiwa wametoka kutoa sare na vinara wa ligi mtibwa sugar katika uwanja wa manungu.

Katika misimu miwili iliyopita simba sc hawajawahi kupata matokeo ya ushindi mbele ya kagera sugar zaidi ya sare, hivyo leo jioni wanakibarua cha kuondoa jinamizi linalo wasumbua mbele ya kagera sugar.

Kocha wa kagera sugar Salum Mayanja amejinadi kikosi chake kipo teyari kupata matokeo katika uwanja wa taifa, akisema atishwi na usajili ambao simba sc wameufanya.

Wakati kocha wa Simba sc Patrick Phiri amenukuliwa na vyombo vya habari mbalimbali akisema kikosi chake teyari kimeiva kwa ajili ya mchezo wa leo na mbio za kusaka ubingwa wa bara
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.