RONALDO MCHEZAJI BORA WA MWAKA 2014



Ikiwa zimebaki takribani wiki mbili kabla ya kutolewa kwa tuzo za FIFA kwa wachezaji waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka huu wa 2014 unaomalizika hivi karibuni,baadhi ya wachambuzi wa soka wameanza kutoa tathimini yao.

Tuzo maarufu zaidi kwa mchezaji bora wa kiume(Ballon d'or) ambayo inawaniwa vikali na Lionel Messi,Cristiano Ronaldo na Manuel Neuer inaonekana kuwa kivutio siku zote.



Nyota hao watatu ambao walifanya vizuri zaidi katika mwaka huu wameingia katika hatua hiyo ya tatu bora kufuatia kupata kura zaidi katika kinyang'anyiro hicho.

Messi hakufanikiwa kupata kikombe chochote na Barcelona lakini aliweza kuisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Dunia huku akifanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora wa kampeni hizo.



Ronaldo alifanikiwa kufunga magoli 61 kati ya michezo 61 aliyoichezea Real Madrid na timu yake ya taifa ya Ureno huku akiisaidia klabu yake kushinda taji la Ligi ya mabingwa barani Ulaya,Kombe la Uhispania(Copa Del Rey) na Kombe la Klabu Bingwa Dunia.



Neuer ambaye ni mlinda mlango mahiri wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani aliweza kuisaidia klabu yake kutwaa taji la Bundesliga na Kombe la Ujerumani(German Cup) huku akifanikiwa kushinda taji la Kombe la Dunia na akipewa tuzo ya kipa bora wa michuano hiyo iliyofanyika nchini Brazil.



Timu ya wachambuzi wa soka katika kituo cha ESPN ilitabiri kwamba nyota wa Ureno na klabu ya Real Madrid,Cristiano Ronaldo ana nafasi nzuri zaidi ya kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Dunia(Ballon d'or 2014). Tuzo hizo zinataraji kutolewa Januari 12 ya mwaka 2015 mjini Zurich yalipo makao makuu ya shirikisho la soka la dunia(FIFA)
chanzo: kandanda
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.