OKWI KUWA KOSA KAGERA SUGAR
MSHAMBULIAJI Elias Maguri wa Simba akitafuta mbinu za kumtoka beki Oscar Joshua wa Yanga.
Habari za uhakika kutoka Zanzibar ilipo kambi ya Simba, zinaeleza Okwi anataka apate fursa ya kuadhimisha siku yake ambayo ni kesho kwa kupumzika hadi kesho kutwa.
Okwi amesaini mkataba wa kuichezea Simba kwa miaka miwili baada ya ule wa awali aliojifunga kwa miezi sita kufikia tamati.
Kwa upande wa Maguri, aliyetua Simba kutoka Ruvu Shooting, hataonekana uwanjani kuwavaa Kagera kutokana na kuwa majeruhi.
“Maguri hatakuwepo, lakini Okwi anataka apate ruhusa asicheze kwa sababu kesho ni siku yake ya kuzaliwa. Angependa kupumzika kesho na kesho kutwa ambayo mechi hiyo itachezwa,” alisema mtoa habari ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba aliyeomba hifadhi ya jina lake.