MTOTO WA MIAKA MITATU AMEATHRIKA KWA DAWA ZA KULEVYA
Zena akiwa na mtoto wake.
Mtoto mwenye umri wa miezi mitatu, mkazi wa Buza, Dar es Salaam amebainika kuwa mwathirika wa dawa za kulevya.
Damu
na mkojo vya mtoto huyo (jina tunalihifadhi) vilichukuliwa na kupimwa
katika maabara ya Hospitali ya Mwananyamala na baada ya saa mbili,
majibu yalitoka na kuthibitisha kwamba alikuwa na chembechembe za dawa
za kulevya aina ya heroini.
Taarifa
za kitabibu zinaonyesha kuwa kuwapo kwa heroini mwilini mwa mtu, huweza
kuonekana katika mkojo ndani ya siku mbili hadi nne iwapo dawa hizo
zilitumiwa na mhusika kwa kati ya saa mbili hadi tano.
Hatua
ya kumfanyia vipimo mtoto huyo wa kiume, inatokana na jitihada za
gazeti hili kutaka kufahamu jinsi utumiaji wa dawa za kulevya kwa
wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha unavyoweza kumwathiri mtoto
akiwa tumboni au anayenyonya maziwa ya mama mwathirika.
Mtaalamu
wa tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Elifasi Mritu anasema: “Ni
kweli ukitumia dawa za kulevya wakati unanyonyesha au wakati wa mimba,
mtoto naye huathirika.”
Kauli
ya Dk Mritu ambaye ni daktari katika kitengo cha tiba ya methadone
hospitalini hapo, inaungwa mkono na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya
Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Frank Mushi ambaye
anasema mama anayetumia dawa za kulevya akiwa mjamzito humwathiri pia
mtoto.
Mama wa mtoto azungumza
Mama
wa mtoto, Zena maarufu Zerish, mkazi wa Yombo Buza alikiri kwamba
alipata ujauzito wakati akitumia dawa za kulevya na kwamba hadi sasa
anavuta dawa hizo huku akiendelea kumnyonyesha mtoto huyo.
Anasema
baada ya kujifungua hakukaa ndani kwa siku 40 kama wafanyavyo wanawake
wengi wa Kitanzania, kwa sababu mwili wake ulikuwa unahitaji ‘unga’
vinginevyo hali yake huwa mbaya.
Anasema
baada ya kujifungua alianza kuzunguka huku na kule akiwa na mtoto
mgongoni, huku akiwa amebeba mfuko wake wa plastiki wenye mahitaji
muhimu ya mtoto kama nepi na nguo.
Anasema
anapovuta au kujichoma dawa, mtoto wake pia hupata ‘stimu’ kwa sababu
hupata dawa hizo za kulevya kupitia maziwa anayonyonya na hivyo wote
wawili kulala fofofo sehemu yoyote ile.
Hata
hivyo, kwa Zerish na mwanaye, anapofikia hali ya kuwa ‘alosto’ (wakati
dawa za kulevya zinapoisha mwilini na hivyo kuhitaji tena), huwa ni
adhabu kali mno.
Anasema
dawa zinapoisha mwilini na mtoto naye huwa katika hali hiyo na hivyo
hulia sana. Hali hiyo humfanya akimbie kutafuta dawa ili ‘kujinusuru’
yeye na mwanaye.
Uwezekano wa tiba
Dk
Mushi anasema watoto wanaoathirika kwa dawa kupitia mama zao, hulia
sana na kujinyonganyonga hali inayoashiria wanapata maumivu ya tumbo.
“Lakini
tumaini lipo kwa watoto hao, kwani hupewa dawa aina ya morphin ambayo
hukata ulevi huo taratibu. Baada ya muda hupona kabisa,” anasema.
Hata
hivyo, alisema iwapo mtoto ataendelea kunyonya maziwa bila kupata tiba
huku mama naye akitumia dawa hizo, huweza kuwa mtumiaji wa dawa hadi
anapokuwa mkubwa.
Katika
hospitali za Muhimbili na Mwananyamala, wanawake wenye watoto walio na
uraibu wa dawa za kulevya hutakiwa kuhudhuria kliniki kila siku bila
kukosa.
Mwanamke anayetumia dawa za kulevya hutibiwa kwa dawa aina ya methadone na mtoto hupewa morphin