MBUNGE WA JIMBO LA MBEYA MJINI ATELEKEZA FAMILIA YAKE
Aliyekuwa
mpenzi wake na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, Faiza
Ally amemtupia mzazi mwenzake kuwa hamjali mwanae baada ya kuachana.
Faiza alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV ambapo alikiri kuwa kuachana na Sugu kunaendelea kumuumiza.
“Imeniathiri
sana hata hailezeki,” alisema. “Naona hata nikieleza siwezi kumaliza.
Imeniathiri kiasi kikubwa sana, kwa sababu na mwaka mzima kama
nikipumzika kulia ni siku moja.”“Yaani inauma sana mtu ambaye ulikuwa
unamuona wakati wote unaomtaka, ukimpigia simu saa yoyote hata kama
akiwa kazini, akiwa bungeni labda lazima akiona simu yako hata akiwa
hawezi kupokea lazima aku-text kwamba nitakupigia nipo kwenye situation
hii. Lakini inafika wakati nikimpigia hapokei na hata ukimtumia meseji
anakujibu baada ya siku kadhaa. Kwahiyo mimi imefika wakati nimeona
kwamba hajali kwa sababu haiwezekani ukae miezi miwili mitatu hujamuona
mtoto na usimpigie simu hata kusikia sauti yake,” aliongeza.

