MAITI YA FUNGIWA NDANI SIKU NNE ASKARI WAINGILIA KATI KUTOA MWILI HUO
Mtu
mmoja Timotheo kweka (30) mkazi wa kiwanja cha ndege manispaa ya
Morogoro amekutwa chumbani kwake amefariki dunia siku nne ziizopita na
jeshi la polisi limelazimika kuvunja mlango na kutoa mwili huo .
Akizungumza
na ITV mmiliki wa nyumba alikokuwa amepanga Leonard Benedicti amesema
kwa mara ya mwisho marehemu alionekana nje siku ya jumamosi hadi leo
walipohisi harufu nzito chumbani kwake ndipo walitoa tarifa kwa jeshi la
polisi na kumkuta ndani amefariki na kichwa kikiwa kimebanwa kwenye
stuli.
Wakizungumzia
tukio hilo ndugu wa marehemu wamesema hawanawasiwasi na kifo cha ndugu
yao kwani alikuwa mlevi wa pombe kwa muda mrefu ambapo wamesema siku ya
jumamosi walikuwa na sherehe ya ukoo lakini marehemu hakuweza kufika
ingawa hawakujua kama amefariki.
Jeshi
la polisi mkoa wa Morogoro limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo
mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika
hospitali ya mkoa wa morogoro.