The site for daily Tanzania Hard News and Entertainment
Home/Entertainment/Events/Politics/MAAJABU YA UCHAGUZI 2015 MGOMBEA MMOJA KUPOTEZA MAISHA WAKATI WA KAMPENI SOMA HAPA UJUE NI NANI HUYO
MAAJABU YA UCHAGUZI 2015 MGOMBEA MMOJA KUPOTEZA MAISHA WAKATI WA KAMPENI SOMA HAPA UJUE NI NANI HUYO
Mrithi
wa Mnajimu na Mtabiri wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Marehemu
Sheikh Yahya Hussein, Alhaj Maalim Hassan Yahya Hussein, ametabiri
kwamba kiongozi mmoja mzee aliye kwenye kinyang’anyiro cha kuwania
urais, atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufa mwakani. Amesema kiongozi huyo, ambaye hakumtaja jina, atafariki dunia baada ya tukio hilo wakati akikimbizwa hospitali.
Alitangaza
utabiri huo, alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam
jana, kuhusu kutumia kwa utabiri alioutangaza mwaka 2014, uchaguzi mkuu
na utabiri wa mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka 2015.
“Kiongozi
mmoja mzee kwa umri ambaye yumo kwenye sakata la urais atadondoka
ghafla kwenye jukwaa na kufa akikimbizwa hospitalini,” alisema Maalim
Hassan.
Pia alisema kwa mwaka mpya wa 2015 kuanza siku ya
Alhamisi, kunaashiria wazee maarufu na hasa wale walio katika uongozi au
waliokuwa viongozi kufariki kwa wingi na kwa hilo akasema: “Mtaona
ajabu yake.”
Vilevile, alitabiri mwaka 2015 kwamba utakuwa wa
shida kubwa kwa familia, ambazo iwapo wahusika hawatafanya juhudi za
kuangalia watoto wao, vifo vya ajabu vitatokea ndani ya familia zao.
Pia alitabiri mwaka 2015, wizi utakuwa mwingi na wezi watauawa na udhalimu wa madhalimu utabainika na kuumbuka.
Aidha,
alitabiri mwaka 2015 kushuhudia uongo mwingi wa kutisha hasa kutoka kwa
viongozi wa kidini na kisiasa pamoja na wanawake wenye nyadhifa au
maarufu katika jamii
Pia alitabiri mwaka 2015 utamweka wazi
kiongozi mmoja mashuhuri wa siasa nchini kurukwa kwake kwa akili bila
kufichwa au kusitiriwa kama ilivyokuwa katika mwaka 2014.
Alisema katika mwaka 2014, kiongozi huyo alikumbwa na mkasa huo, lakini suala hilo likafanywa kuwa siri kubwa.
Pia
alitabiri misiba miwili ya kitaifa kutokea nchini mwaka 2015 kwa mujibu
wa nyota na kwamba, kuna kiongozi mmoja wa kidini atakumbwa na kashfa
ya mwaka itakayomsababishia anguko kubwa na la aibu.
Kadhalika,
alitabiri viongozi wawili wa siasa na dini kwamba watakumbwa na kashfa
ya ngono, ambayo itawasababishia anguko la utumishi wa kutukuka na
familia zao.
Pia alitabiri mwandishi mmoja mashuhuri nchini
atakumbwa na umauti wa utata utakaoitesa serikali na familia yake
kutafuta suluhu.
Alisema mwaka 2015 utakuwa wa viongozi kuzama
kisiasa na kukumbwa na kashfa kubwa zitakazowaondoa madarakani, ikiwa na
maana kwamba viongozi wanaofahamika wataanguka kiuchumi, kisiasa,
kibiashara na kijamii.