KWELI HAKI HAIOBWI BALI INATAFUTWA JAMAA AVAA GUNIA NA KUINGIA OFISINI KUDAI CHAKE
Na Johnson James, Mwanza
MKURUGENZI wa Jiji la Mwanza, Halifa Hassan Hida ameingia katika kashfa nzito baada ya mwanaharakati aliyefahamika kwa jina la John Masweta kutinga kwenye geti kuu la Makao Makuu ya Jiji la Mwanza jana huku akiwa amevaa gunia kumshinikiza mkurugenzi huyo amlipe shilingi 1,600,000 aliyopewa kama zawadi na uongozi wa mkoa na mkurugenzi huyo kushindwa kuilipa fedha hiyo kwa wakati.
MKURUGENZI wa Jiji la Mwanza, Halifa Hassan Hida ameingia katika kashfa nzito baada ya mwanaharakati aliyefahamika kwa jina la John Masweta kutinga kwenye geti kuu la Makao Makuu ya Jiji la Mwanza jana huku akiwa amevaa gunia kumshinikiza mkurugenzi huyo amlipe shilingi 1,600,000 aliyopewa kama zawadi na uongozi wa mkoa na mkurugenzi huyo kushindwa kuilipa fedha hiyo kwa wakati.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Mwanza kwenye lango kuu la kuingia ofisi
za jiji hilo, Masweta alisema kuwa yeye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tanzania Environment & Conservation (TECO)
aliyejitolea kwa zaidi ya miaka 20 kupanda miti na amekuwa akipewa tuzo
mbalimbali kutokana na kazi hiyo na kuweza kuliokoa taifa katika
majanga ya jangwa.
Masweta
ameendelea kufafanua kuwa katika kuhakikisha analisaidia taifa,
amepanda miti katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza na wakati
akiendelea kupanda miti hiyo akawa amepatiwa tuzo ya mwanaharakati bora
kwa kutunza mazingira iliyoambatana na fedha taslimu shilingi milioni
moja na laki sita lakini cha kushangaza mkurugenzi amekataa kutoa fedha
hiyo na badala yake amempatia cheti tu bila kumpatia na fedha.
Katika
hatua nyingine, Masweta ameendelea kusema kuwa yeye hakupanda miti kwa
lengo la kulipwa na taifa bali alipanda miti ili kuliondoa taifa
katika janga la kukumbwa na jangwa lakini cha kushangaza kila
anapotiwa moyo kwa kupatiwa fedha kidogo, fedha hiyo huishia mikononi
mwa watu wengine ambao hawana huruma na maisha yake.
Hata
hivyo, Masweta alikuwa na mabango yaliyoandikwa ujumbe mbalimbali
kama Toa nguvu zako kwa kulitumikia taifa, uwe faida kwa jamii na
taifa, onea huruma tumbo lako kula mpaka sisimizi, Udhalimu wa
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza haukubaliki.
Masweta amesema kuwa hatoki kwenye lango hilo hadi pale mkurugenzi huyo atakapompatia kiasi hicho cha fedha anazodai.
Aidha
Masweta ametoa rai kwa raia kwa kusema kuwa yeye ni mgonjwa wa
kisukari na hajanywa maji yoyote tokea asubuhi endapo akifariki basi
wafahamu kwamba aliyesababisha kifo chake ni Mkurugenzi wa Jiji la
Mwanza kutokana na kuwa na nia ya kudhulumu haki za wenzake.