KIJANA AJINYONGA UKWENI BAADA YA KUKATALIWA
Mkazi
mmoja wa Kijiji cha Nyamisisi, Kata ya Kukirango, wilayani Butiama,
Ryakora Kurwijira (34) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia shati lake
akiwa ukweni baada ya kukataliwa na mkewe aliyekuwa akiishi naye.
Habari
zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa karibu, zinaeleza kwamba marehemu
alikuwa akiishi na mkewe aitwaye Doy Nyanyara katika Kijiji cha Nyatwari
wilayani Bunda kwa kipindi cha miaka miwili, lakini ghafla mwanamke
huyo alimfukuza marehemu kutoka nyumbani na kumwambia kuwa amepata mume
mwingine wa kuishi naye, hivyo hamhitaji tena. Wawili hao walikuwa
wakiishi nyumba ya mwanamke.
“Baada ya marehemu kufukuzwa na mkewe aliondoka bila kuaga Jumamosi iliyopita na kwenda nyumbani kwa wazazi wa mwanamke huyo huko Bariadi, Simiyu na kujinyonga kwenye mti pembeni ya nyumba ya baba mkwe wake.
“Alipokaguliwa baada ya polisi kufika alikutwa na ujumbe unaosema: “Nimejinyonga kwa ajili ya kupenda,” kilisema chanzo hicho.
Imedaiwa kuwa baada ya mwanaume huyo kujinyonga, wazazi wa mwanamke huyo walitokomea kusikojulikana, ambapo mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Bariadi kabla ya mwanamke huyo kuwapigia simu ndugu wa marehemu na kuwaambia kuwa ndugu yao amejinyonga.
Ndugu
hao walifuatilia mwili huo na kuukuta katika hospitali hiyo na
kuuchukua kwenda kwao Kiabakari ambako mazishi yalifanyika Desemba 19
mwaka huu.
Afisa mmoja wa polisi wa Bariadi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
Afisa mmoja wa polisi wa Bariadi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo